Ardhi ya Zulani EPS 4

KWENYE SEHEMU HII:

“Nitaishije mwaka mzima katika mji huu wa laana? Mwaka mmoja? Sikuweza hata kuishi siku moja salama! Vipi nikiwa mimi ndiye nitakayekuwa masikini zaidi ifikapo hiyo Siku ya Zulani? Vipi nikiwa mimi ndiye nitakayechinjwa?”

Endelea…

Habil aliinua sauti yake zaidi, akijaribu kuonyesha ujasiri ambao kiukweli

hakuwa nao..,

 “Ndiyo, nitatoka! Lazima nitoke! Fungua hili lango!”

Mlinzi yule hakusumbuka hata kujibizana naye sana. Alimtazama Habil kama mdudu mdogo, kisha akamwambia.., 

“Sisi huacha sherehe za Zulani ziendelee na kusimama hapa kulinda lango kwa sababu moja tu… tunajua walevi kama wewe watakuja hapa kusumbua.”

“Mimi siyo mlevi! Mimi siyo mlevi!” Habil alifoka, akisukuma mkono wa mlinzi yule kwa hasira.

Kitendo hicho kilikuwa kosa kubwa. Uso wa mlinzi ulibadilika na kuwa wa

kikatili.. Bila onyo, mlinzi huyo alirusha ngumi nzito kama jiwe iliyotua moja kwa moja kwenye uso wa Habil.. Ngumi hiyo ilimrusha Habil hewani na kumwangusha vibaya mgongoni. Damu moto ilianza kumtiririka kutoka kwenye nyusi yake ya kushoto na mdomoni.

Habil alijaribu kuinuka haraka, ingawa dunia ilikuwa ikimzunguka. Alisimama tena mbele ya mlinzi yule, akitaka kupambana. Lakini ghafla, macho yake yalitua kwenye ngao ya chuma iliyong’aa kifuani mwa mlinzi huyo, iliyokuwa kama kioo.

Habil aliiona sura yake mwenyewe kwenye ngao ile. Alishtuka. Macho yake yalipanuka kwa hofu, na mapigo ya moyo yalimwenda mbio.

🔒

Kipindi Hiki Kimefungwa

Ili kuendelea kusoma riwaya hii nzuri, tafadhali ingia kwenye akaunti yako.
Kama ni mara yako ya kwanza kufika hapa, tunakukaribisha kujisajili!

5 1 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
bwengo
bwengo
2 hours ago

unyama sana hii hadithi👌👌

You cannot copy content of this page

1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x