Ardhi ya Zulani EPS 3

Habil alitembea kuelekea upande ule aliouonyesha yule mwanaume. Alisonga mbele mpaka alipofika ukingoni mwa bonde kubwa lenye Uwanda wa juu. Aliposimama ukingoni na kutazama chini, macho yake yalipanuka kwa mshangao uliochanganyika na udadisi.

Kule chini kabisa, kulikuwa na mji mkubwa na wenye muonekano wa kuvutia mno.

Majengo yake yalipangwa kwa ustadi, yakizingirwa na maeneo mapana ya kijani

kibichi yenye mimea, miti mirefu, na mito ya maji iliyopita katikati yake, kana

kwamba ni ardhi ya paradiso iliyofichwa katikati ya jangwa. Ilikuwa ni Zulani.

Macho ya Habil yalimtoka kwa mshangao mkuu. Moyo wake ulidunda kwa kasi ya

ajabu akiwa amesimama ukingoni mwa lile bonde. Akili yake ilikataa kabisa

kuamini kile alichokuwa anakiona. Aliendelea kujiuliza kimoyomoyo

“Inawezekanaje mji mzuri na mkubwa namna hii kuwepo katikati ya jangwa hili la kifo? Je, nipo kwenye ndoto? Au lile handaki limenisafirisha kwenda sayari nyingine?”

Wale wanaume wawili aliokutana nao jangwani walikuwa wamesha tokomea mbali, lakini maneno yao yaliendelea kurejea masikioni mwake: “Inaonekana hujui chochote… Sisi ni masikini tunaokimbia ardhi ya Zulani.”

🔒

Kipindi Hiki Kimefungwa

Ili kuendelea kusoma riwaya hii nzuri, tafadhali ingia kwenye akaunti yako.
Kama ni mara yako ya kwanza kufika hapa, tunakukaribisha kujisajili!

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted

You cannot copy content of this page

0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x