Makubaliano ya Mtumiaji

Masharti na Vigezo (Terms of Service)

Ilisasishwa Mwisho: Septemba 2026 | Inatumika kwenye duniaxpose.com

Karibu DuniaXpose. Kwa kutumia, kutembelea, au kusoma riwaya na maudhui yaliyopo kwenye tovuti hii (duniaxpose.com), unakubali kufuata na kufungwa na Masharti na Vigezo hivi. Tafadhali yasome kwa makini kabla ya kuendelea kutumia huduma zetu.

1. Matumizi ya Tovuti

Unakubali kutumia tovuti hii kwa malengo halali ya kisheria pekee. Ni marufuku:

  • Kujaribu kuharibu, kudukua, au kuingilia mifumo ya kiufundi na kanzidata ya DuniaXpose.
  • Kutumia roboti au programu za kiotomatiki (web scrapers) kunakili hadithi au maudhui yetu bila idhini ya kimaandishi.
  • Kutoa maoni yenye lugha ya matusi, uchochezi, au yanayokiuka utu wa watu wengine.

2. Hakimiliki na Umiliki wa Maudhui (Copyright)

Riwaya zote, hadithi za vipindi, makala, nembo, michoro na majalada yaliyopo kwenye DuniaXpose ni mali halali ya DuniaXpose na waandishi husika, yakilindwa na sheria za hakimiliki za ndani na kimataifa.

Tanbihi ya Hakimiliki: Huruhusiwi kunakili, kusambaza, kuuza upya, au kuchapisha sehemu yoyote ya riwaya zetu kwenye majukwaa mengine (kama vile WhatsApp, Facebook, Telegram, au blogu nyingine) bila idhini rasmi.

3. Mfumo wa Token na Usomaji wa Riwaya

  • Akaunti na Salio: Mtumiaji anapaswa kufungua akaunti ili kupata pochi ya kidijitali (Wallet) kwa ajili ya kuweka na kutumia token kusoma vipindi.
  • Ukomo wa Token: Token zikishanunuliwa hutumika kufungua vipindi vilivyolipiwa ndani ya tovuti na haziwezi kubadilishwa kuwa pesa taslimu (non-refundable) pindi muamala unapokamilika.
  • Usalama wa Akaunti: Una wajibu wa kutunza siri ya nenosiri lako. Shughuli zote zinazofanyika chini ya akaunti yako zitakuwa chini ya uwajibikaji wako.

4. Matangazo ya Washirika (Google AdSense & Third Parties)

Tovuti ya DuniaXpose inaweza kuonyesha matangazo yanayotolewa na Google AdSense au mitandao mingine ya matangazo ya wahusika wengine. Wasomaji wanatakiwa kuelewa kwamba watangazaji hawa wanaweza kutumia vidakuzi (cookies) kulingana na sera zao wenyewe.

DuniaXpose haihusiki na miamala au makubaliano yoyote unayofanya na tovuti au huduma unazoziona kupitia viungo vya matangazo hayo.

5. Ukomo wa Dhima (Disclaimer)

Hadithi na riwaya zetu ni kazi za kubuni (fiction). Majina, wahusika, na matukio yanayotajwa yanatumika kiubunifu na hayalengi kumkashifu au kumuakisi mtu yeyote halisi, aliye hai au aliyetangulia mbele ya haki.

6. Mabadiliko ya Masharti

DuniaXpose ina haki ya kurekebisha au kusasisha Masharti na Vigezo hivi wakati wowote ili kuendana na mabadiliko ya kisheria au ya kiufundi. Toleo lililosasishwa litawekwa wazi kwenye ukurasa huu.

Maswali Kuhusu Masharti Yetu: Kama una maoni, mapendekezo, au maswali kuhusu vigezo hivi, wasiliana nasi kupitia:

You cannot copy content of this page